Ni kufuatia uchunguzi kuhusu mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel yaliyolenga na kuua mamia ya wafanyakazi wa mashirika ya kimataifa na taasisi za kutoa misaada huko Ghaza.
Kanzidata ya "Responsible Statecraft", ambayo ni ya taasisi ya wanafikra ya Marekani "Quincy", imechapisha makala inayozungumzia mashambulizi ya utawala wa Kizayuni wa Israel dhidi ya wafanyakazi wa mashirika ya misaada huko Gaza, ikichunguza kesi 14 za mashambulizi hayo, ambayo ushahidi unaonyesha kuwa, yalifanyika kwa makusudi.
Taasisi hiyo ya Marekani imesisitiza kuwa, uchunguzi wa mashambulizi ya Israel dhidi ya mashirika haya umefichua mwenendo usio wa kibinadamu.
Kwa mujibu wa ripoti hiyo, tangu Oktoba 7, 2023, jumla ya wafanyakazi 378 wa misaada ya kibinadamu wameuawa duniani kote, 75% kati yao wakiwa wa Gaza au Ukingo wa Magharibi huko Palestina inayokaliwa kwa mabavu.Takwimu zinaonyesha kuwa idadi ya wafanyakazi wa misaada waliouawa na Israel huko Palestina katika miezi mitatu ya mwishoni mwa mwaka 2023 ni zaidi ya idadi ya wafanyakazi wa misaada waliouawa katika maeneo mengine ya dunia katika mwaka huu.
342/